Posts

Showing posts from July, 2022
Image
  Na John Mapepele, Birmingham Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola   Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona ili kurejea na medali. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa kwa ujumla. "Nawaomba tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita  tunahitaji kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha,  amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua  na kuendeleza michezo kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa. " kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali  imeamua kutoa fedha nyingi kwa w...

Waziri Mchengerwa aongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania, Birmingham Uingereza

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe,  Mohammed Mchengerwa  ameongoza kikao cha maandalizi ya ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Mawaziri wa Michezo wa Jumuiya ya Madola kitakachoanza leo Julai 26 mjini Birmingham, Uingereza.  Kikao hicho ni maandakizi mahususi kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu yanayofanyika nchini Uingereza huku Tanzania ikiwa imeshiriki katika michezo hiyo. Katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza Serikali imetoa  motisha kubwa kwa wachezaji watakaofanya vizuri na kurejea na tuzo nchini. Mhe. Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha   michezo inatumika kikakamilifu kuitangaza Tanzania kimataifa. Aidha, amesema michezo ni ajira na uchumi mkubwa ambapo amesisitiza wachezaji wote kuwa wazalendo kujituma kufa na kupona kwa ajili ya taifa la Tanzania. Amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuleta mapind...

Mhe. Mchengerwa amwaga vifaa vya michezo shule zote wilaya ya Rufiji, aanzisha ligi ya Sensa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji.  Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote  wanaoshiriki kwenye mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano  ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji. Mhe. Mchengerwa amekabidhi  vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai 17, 2022 kwenye  shule ya Sekondari ya Ikwiriri   Wilaya ya Rufiji ambapo amesema ameamua  kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara  na ajira kubwa  kwa vijana. “Nimeamua kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua  kwa sasa michezo ni miongoni mwa chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi i...

Siku ya kiswahili yafana

Image
  Na John Mapepele Mamia ya wadau leo Julai 7, 2022 wameshiriki maadhimisho ya kwanza ya siku ya Kiswahili duniani jijini Dar es Salaam. Maadhimisho haya  yanafanyika  kwa mara ya kwanza kufuatia  UNESCO kuridhia kiswahili kuwa lugha rasmi kuwa lugha kutumika kimataifa. Mgeni rasmi wa shughuli hii, Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Dkt. Isdor Mpango. Mhe. Mpango mara baada ya kufika ametembelea maonesho ya wadau mbalimbali wa kiswahili ambao wamekuwa wakionesha kazi za kiswahili. Wadau mbalimbali wa kiswahili wametoa mada na shuhuda za ukuaji wa kiswahili kwa lugha ya kiswahili. Washiriki wamepongeza kwa watoa mada na mashuhuda wote kutoka ndani na nje ya Tanzania waliopanda kuzungumza kwa kusema vizuri lugha ya kiswahili. Kaulimbiu  ya siku hii ni " kiswahili ni chachu ya maendeleo na utengamano duniani "

Mchengerwa- Mkakati wa kubidhaisha kiswahili kuzinduliwa siku ya kiswahili duniani

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kesho  katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani Serikali inakwenda kuzindua Mkakati wa kukuza na kubidhaisha lugha ya Kiswahili wa miaka kumi kuanzia 2022 hadi 2032. Amesema mgeni rasmi katika siku ya kilele cha siku ya kiswahili duniani  anatarajiwa kuwa Makamo wa Rais, Mhe. Isdor Mpango. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Julai 6, 2022 kwenye mdahalo wa kujadili mchango wa kiswahili katika ukombozi wa nchi za Afrika wakati akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau. Amesema pamoja na mambo mengine mkakati huo utajikita katika eneo la uandaaji wa kanzidata na maeneo ya wataalam, kutafuta fursa za kiswahili na kuwaunganisha  nazo. Aidha, amesema lazima kama Serikali lazima kuongeza weledi na kuamua tunataka  kufanya nini ili dunia ijue kuwa kiswahili kilizaliwa Tanzania  na kunufaika nacho. "Pale viongozi wanapokwenda katika mataifa mbalimbali dunia...
Image
  Na John Mapepele. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ametoa vifaa vya michezo kwa timu zote 45 zinazoshiriki mashindano ya kombe la Yamleyamle Zanzibar ili timu ziweze kufanya vizuri hatimaye  kuwapata wachezaji bora na wenye  vipaji ambao wataunganishwa  kwenye timu ya Taifa. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Julai 3, 2022 wakati akizindua mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar ambapo amesema Mhe. Rais ametoa mipira 45 kwa ajili ya timu hizo na jezi. “Niwaombe  tunapojipanga kwenda kuandaa mashindano ya AFCON,  tuleteeni orodha  ya  vijana wanaofanya vizuri tutahakikisha tunawaingiza kwenye time zetu za taifa, tutawaendeleza, tutakuza vipaji vyao kwa maslahi  ya Serikali zote mbili SMT na SMZ”. Amesisitiza Mhe, Mchengerwa. . Amewapongeza kwa kuandaa mashindano hayo ambapo amefafanua kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaa...

Mhe. Mchengerwa- Serikali kumwaga studio kila Wilaya nchini

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali inakwenda  kutengeneza studio kila wilaya kwa ajili ya kurekodia kazi za sanaa. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 3, 2022 wakati akifunga tamasha la kwanza la  kitaifa la utamaduni katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Aidha amesema wizara yake inakwenda  kutekeleza maelekezo ya viongozi wetu ya kuthamini, kuandaa  mavazi ya taifa ili kuhakikisha mila na desturi za mtanzania zinaendelezwa. " Maelekezo ya viongozi wetu ni sheria, amri iwe jua, iwe mvua  sisi Wizara, tutawajibika kutekeleza bila kusita wala kuchelewa" amesisita Mhe. Mchengerwa Pia amesema  wizara imejipanga vizuri kuhakikisha Tamasha la kitaifa la pili la Utamaduni litakalofanyika mwakani litakuwa katika kiwango cha kimataifa. Ameongeza kuwa kumalizika  kwa tamasha hili ni mwanzo wa kuanza maandalizi ya matamasha kwenye mikoa  na wilaya zote nchini ambapo ametaka maa...

Watu zaidi ya milioni kumi washuhudia Tanzania Utamaduni Carnival leo

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  watu zaidi ya milioni kumi wameshuhudia matembezi ya kiutamaduni  katika jiji la Dar es Salaam. Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kwenye uzinduzi wa tamasha la kwanza la kitaifa la Utamaduni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua kuwa idadi hiyo inatokana na watu walioshiriki moja kwa moja na wale walioangalia kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Amesema kufanyika kwa tamasha hili la kwanza la kitaifa la utamaduni ambalo limejumuisha  matembezi  ya kiutamaduni ni maono ya Mhe.Rais ya kutaka kukutanisha utamaduni wetu. Ameongeza kuwa upekee wa tamasha  hili ni kuwa limeandaliwa mahususi kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya kiswahili duniani. Aidha, amefafanua kuwa Taifa lisilo na mila na desturi ni sawa na taifa lililo mateka na mufu. Amemthibitishia,  Mhe. Majaliwa, kuwa maelekezo aliyoyatoa kuhusian...