Watu zaidi ya milioni kumi washuhudia Tanzania Utamaduni Carnival leo

 

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  watu zaidi ya milioni kumi wameshuhudia matembezi ya kiutamaduni  katika jiji la Dar es Salaam.

Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kwenye uzinduzi wa tamasha la kwanza la kitaifa la Utamaduni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua kuwa idadi hiyo inatokana na watu walioshiriki moja kwa moja na wale walioangalia kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema kufanyika kwa tamasha hili la kwanza la kitaifa la utamaduni ambalo limejumuisha  matembezi  ya kiutamaduni ni maono ya Mhe.Rais ya kutaka kukutanisha utamaduni wetu.

Ameongeza kuwa upekee wa tamasha  hili ni kuwa limeandaliwa mahususi kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya kiswahili duniani.


Aidha, amefafanua kuwa Taifa lisilo na mila na desturi ni sawa na taifa lililo mateka na mufu.

Amemthibitishia,  Mhe. Majaliwa, kuwa maelekezo aliyoyatoa kuhusiana na kuwa na mavazi ya taifa  anakwenda kuyatekeleza mara moja.

Amesema Machifu takribani  50 wameshiriki katika tamasha hili ambapo amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaheshim na kuwatetea Viongozi hao wa kimila.

Aidha amewashukuru machifu kujitoa kwenye  shughuli mbalimbali za Serikali hususan zoezi la kitaifa  la sensa litakalifanyika Agosti 23, 2022.

Amesema tamasha hili ni la kipekee kwa kuwa limeshirikisha takribani mikoa yote ya Tanzania na limeshirikisha  Utamaduni Carnival, usiku wa taarabu ambao utafanyika kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam Julai 3, 2022.

Ametoa wito kwa watu wengi kujitokeza  kwa wingi kwenye usiku wa taarabu kwa kuwa hakuna kiingilio.


Comments

Popular posts from this blog

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA-MHE MCHENGERWA

Diamond apongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuwasaidia wasanii, kurejesha tuzo

Rais Samia Aipongeza Wizara Ya Utamaduni, Sanaa Na Michezo Kwa Mikakati Na Ubunifu Mkubwa.