Siku ya kiswahili yafana
Na John Mapepele
Mamia ya wadau leo Julai 7, 2022 wameshiriki maadhimisho ya kwanza ya siku ya Kiswahili duniani jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho haya yanafanyika kwa mara ya kwanza kufuatia UNESCO kuridhia kiswahili kuwa lugha rasmi kuwa lugha kutumika kimataifa.
Mgeni rasmi wa shughuli hii, Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Dkt. Isdor Mpango.
Mhe. Mpango mara baada ya kufika ametembelea maonesho ya wadau mbalimbali wa kiswahili ambao wamekuwa wakionesha kazi za kiswahili.
Wadau mbalimbali wa kiswahili wametoa mada na shuhuda za ukuaji wa kiswahili kwa lugha ya kiswahili.
Washiriki wamepongeza kwa watoa mada na mashuhuda wote kutoka ndani na nje ya Tanzania waliopanda kuzungumza kwa kusema vizuri lugha ya kiswahili.
Kaulimbiu ya siku hii ni " kiswahili ni chachu ya maendeleo na utengamano duniani "
Comments
Post a Comment