Mchengerwa- Mkakati wa kubidhaisha kiswahili kuzinduliwa siku ya kiswahili duniani

 


Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kesho  katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani Serikali inakwenda kuzindua Mkakati wa kukuza na kubidhaisha lugha ya Kiswahili wa miaka kumi kuanzia 2022 hadi 2032.

Amesema mgeni rasmi katika siku ya kilele cha siku ya kiswahili duniani  anatarajiwa kuwa Makamo wa Rais, Mhe. Isdor Mpango.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Julai 6, 2022 kwenye mdahalo wa kujadili mchango wa kiswahili katika ukombozi wa nchi za Afrika wakati akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau.

Amesema pamoja na mambo mengine mkakati huo utajikita katika eneo la uandaaji wa kanzidata na maeneo ya wataalam, kutafuta fursa za kiswahili na kuwaunganisha  nazo.
Aidha, amesema lazima kama Serikali lazima kuongeza weledi na kuamua tunataka  kufanya nini ili dunia ijue kuwa kiswahili kilizaliwa Tanzania  na kunufaika nacho.

"Pale viongozi wanapokwenda katika mataifa mbalimbali duniani lazima waandaliwe ili waweze kukitangaza kiswahili kimkakati" amesisitiza, Mhe. Mchengerwa

Amesema hii tabia ya kusema tunabidhaisha  lugha ya bila ya kuwa na mikakati haitakuwa na tija ikiwa hakutakuwa na jitihada za makusudi za kukitangaza kiswahili ambapo amelitaka  BAKITA  kujipanga zaidi.

Pia amewataka kila anayepata fursa kukitangaza kiswahili afanye kwa weledi ili fursa hizo zitoe majibu.

Amelielekeza BAKITA kutoka na kukielezea kiswahili badala ya kufanya mazoea ya kukaa maaofisini.

Pia amesema Kamusi za lugha ya Kiswahili zisitumike tu kwenda kwenye matamasha bali zifike kwenye mashule ili zitumike  hatimaye kutoa wigo mpana kwa wanafunzi kuelewa lugha ya kiswahili.

Kuhusu kukisamba kiswahili katika balozi mbalimbali duniani amesema tayari  Serikali  imesaini mkataba na nchi ya Afrika ya kusini kwa ajili ya kufundisha katika balozi zake.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wizara , Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amesema anawashukuru wadau wote waliochangia na kwamba michango yao yote itafanyiwa kazi  ili kukuza lugha adhimu ya Kiswahili.

Comments

Popular posts from this blog

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA-MHE MCHENGERWA

Diamond apongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuwasaidia wasanii, kurejesha tuzo

Rais Samia Aipongeza Wizara Ya Utamaduni, Sanaa Na Michezo Kwa Mikakati Na Ubunifu Mkubwa.