MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA) kutoa elimu ya kutosha kwa wadau hususan wabunge kuhusu mabadiliko makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo ya kimuundo na kisekta ili kusaidia kuinua maisha ya wadau wa sekta ya Sanaa nchini. Waziri Mchengerwa ameyasema haya leo Septemba 14, mara baada ya kupitishwa yeye na Naibu wake Mhe, Pauline Gekul na Menejimenti ya taasisi hiyo kwenye kikao cha kujadili rasimu ya kanuni ya uanzishwaji wa Ada kwa vibebea kazi za ubunifu (blank device) na uanzishwaji wa makampuni binafsi ya wasanii ya ukusanyaji na ugawaji mirahaba (CMO). Amewataka kuharakisha mchakato wa kukamilisha rasimu hizo ili zisainiwe na kuanza kutumika mara moja hatimaye wasani na wadau mbalimbali wa kazi za Sanaa waweze kunufaika na kazi zao. "Harakisheni, ninakwenda kuisaini kanuni hizi mara moja ili wasanii wafaidi matunda ya...