KUPOKEA TAARIFA YA KUSIMAMIA HAKIMILIKI NA UGAWAJI WA MIRAHABA NA MASHUJAA WA JUMUIYA YA MADOLA

 


                    Na Mwandishi wetu– Dodoma 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kesho Agosti 12, 2022, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kupokea  taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Ugawaji wa  Mirahaba kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ya Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzia saa 11 jioni jijini Dar es Salaam. 

Uteuzi wa Kamati hiyo, ulitokana na malalamiko ya wadau hususan wa Sekta ya  Sanaa nchini kuhusiana na namna mirabaha inavyokusanywa na kugawanywa,  kuwepo kwa vitendo vya uharamia katika kazi zao na elimu duni kwa wadau  kuhusu masuala hayo. 

Aidha, uundaji wa Kamati hiyo ulitokana na maelekezo ya Mhe. Rais ya  kuitaka Wizara kusimamia na kutafuta muarobaini wa changamoto za  mirabaha kwa wasanii aliyoitoa Mei 30, 2022 jijini Dar es Salaam. 

Pia, Mhe. Mchengerwa anatarajia kuwakaribisha nyumbani na kuwapongeza  wachezaji mashujaa walioweza kurejea na medali kutoka kwenye Mashindano  ya Jumuiya ya Madola yaliyomalizika hivi karibuni Birmingham nchini Uingereza

Comments

Popular posts from this blog

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA-MHE MCHENGERWA

Diamond apongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuwasaidia wasanii, kurejesha tuzo

Rais Samia Aipongeza Wizara Ya Utamaduni, Sanaa Na Michezo Kwa Mikakati Na Ubunifu Mkubwa.