KUPOKEA TAARIFA YA KUSIMAMIA HAKIMILIKI NA UGAWAJI WA MIRAHABA NA MASHUJAA WA JUMUIYA YA MADOLA
Na Mwandishi wetu– Dodoma Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kesho Agosti 12, 2022, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kupokea taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Ugawaji wa Mirahaba kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ya Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzia saa 11 jioni jijini Dar es Salaam. Uteuzi wa Kamati hiyo, ulitokana na malalamiko ya wadau hususan wa Sekta ya Sanaa nchini kuhusiana na namna mirabaha inavyokusanywa na kugawanywa, kuwepo kwa vitendo vya uharamia katika kazi zao na elimu duni kwa wadau kuhusu masuala hayo. Aidha, uundaji wa Kamati hiyo ulitokana na maelekezo ya Mhe. Rais ya kuitaka Wizara kusimamia na kutafuta muarobaini wa changamoto za mirabaha kwa wasanii aliyoitoa Mei 30, 2022 jijini Dar es ...