Mhe. Mchengerwa apongeza ubunifu wa wadau wa tamasha la Sauti za Busara
Na. John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewapongeza wadau mbalimbali wa Sanaa walioshiriki kwenye tamasha la Sauti za Busara Zanzibar kwa ubunifu wao na kuwataka waendelee kutumia matamasha hayo kutangaza bidhaa na huduma wanazozitoa.
Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo alipotembelea mabanda yaliyokuwa yakionesha bidhaa na huduma zao kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Februari 13, 2022.
Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Mhe. Simai Mohamed Said ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutembelea wadau wa tamasha hilo huku akisisitiza kuwa kitendo hicho kimeonesha anathamini mchango wa wadau hao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said akimtambulisha Mhe. Mchengerwa kwa mmoja wa wadau kwenye banda la Benki ya CRDBMhe. Mchengerwa akiwa na kikosi cha mfalme wa Singeli nchini Sholo Mwamba kabla ya kikosi kupanda jukwaani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said akimpatia zawadi ya fulana Mhe. Mchengerwa wakati alipotembelea kwenye banda la wandaaji
Mhe. Mchengerwa akiangalia kwa makini namna ambavyo kikosi cha Ma DJ kinavyofanya kazi ya kuburudisha umati iliofika kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara, Zanzibar
Comments
Post a Comment