Mhe. Mhengerwa -Tamasha la Sanaa Bagamoyo ni la kimataifa, Makamu wa Rais afafanua kuwa Sanaa inaongoza katika ukuaji wa uchumi nchini
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imefanya maboresho makubwa kwenye Tamasha la mwaka huu la 41 la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo kuwa la kimataifa ambapo limeshirikisha nchi mbalimbali duniani ili kuitangaza Tanzania na utamaduni wake duniani. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais Mhe, Dkt. Philipo Mpango kuzindua rasmi tamasha hili kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano. Mhe. Samia Suluhu Hassan. Ameongeza kuwa tamasha hili limeshirikisha vikundi vya wasanii kutoa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Canada, Zambia, Burundi na Visiwa vya Mayote kutoka nchini Ufaransa. “Mwaka huu tumeendelea kuliboresha Zaidi tamasha hili kutoka kuwa tamasha la mazoea la wanafunzi wa sanaa hapa chuoni ili kulipatia hadhi zaidi ya kuwa tamasha la kimataifa.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha amesema wameteleza maelekezo ya Mhe. Rais ya kutaka kuendeleza tamasha hili n...