Rami Tanzania mwenyeji Tuzo za (MAMA) MTV Africa Music Award 2023
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa Rais na meneja mkuu wa Paramount Africa and Peer Lead BET International, Monde Twala, na kukubaliana kushirikiana katika kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA- MTV Africa Music Award kwa mwaka 2023. Waziri Mchengerwa amekutana na Monde Twala Jijini Los Angeles katika jimbo la California nchini Marekani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022. Katika mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa amemwelezea nia na sababu ya Tanzania kutaka kuwa mwenyeji wa tamasha hilo la utoaji wa tuzo hizo kubwa za burudani kwa Afrika, kuwa ni kuongeza ushawishi kwa vijana wa kitanzania kuendelea kufanya vizuri katika sekta za burudani pamoja na kuitangaza zaidi Tanzania na uzuri wake katika ulimwengu. Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana kuungana kwenye kutafuta washirika katika kuendesha tuzo hizo, na kuridhia kuwa maandalizi yaanze ma...