Mhe Gekul awataka watanzania kutumia fursa za Royal Tour
Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb) amewataka watanzania kutumia fursa iliyotengenezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan kwenye Filamu ya Royal Tour. Mhe. Gekul ameyasema haya leo Aprili 29, 2022 kwenye semina ya wadau wa sekta ya filamu ya Royal Tour katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam. Naibu Waziri Gekul amesisitiza kuwa Serikali Serikali ipo tayari kushirikiana na wanatasnia ya filamu katika kuendeleza Sekta ya filamu nchini ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi yatakayo wawezesha wanatasnia wa ndani na nje ya nchi kufanya shughuli zao nchini. Aidha, amesema yapo maeneo kadhaa muhimu ambayo Tanzania inaweza kushirikiana na Marekani katika filamu na ikanufaika nayo. Ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na utayarishaji wa filamu kwa kutumia mandhari zinazo pat...