Posts

Showing posts from March, 2022

SIKU MOJA YA UPIGAJI KURA TUZO ZA MUZIKI YAONGEZWA- BASATA

Image
  Na. John Mapepele Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) imeongeza muda wa siku mmoja wa kupiga kura kwa ajili ya Tuzo za Muziki 2021 ambapo awali mwisho ulikuwa leo Machi 31, 2022 saa sita usiku na sasa itakuwa hadi Aprili 1, 2022 saa sita usiku, ambapo siku ya utoaji wa tuzo hizo inabaki kama ilivyopangwa Aprili 2, 2022 katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.  Hayo yamesemwa leo Machi 31, 2022 na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Matiko Mniko  kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema  kuongezwa kwa siku hiyo kunatokana na wapenzi wengi wa muziki kuendelea kufurika kupiga kura katika siku hizi za mwisho. “Siku ya kwanza tulitangaza kuwa  mwisho wa zoezi la upigaji wa kura itakuwa leo tarehe 31,3,2022 saa sita usiku lakini kutokana na watu wengi kuonyesha uhitaji katika mchakato huu  tumeona tuongeze siku moja  kutokana na majukumu waliyonayo ili waweze kushiriki na kuwachagua  wasa...

Mchengerwa - Mhe. Rais ameupiga Mwingi kwenye michezo hadi kaondoka nao

Image
  Na. John Mapepele.   Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.  Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Rais Samia ameupiga mwingi hadi ameondoka nao kutokana na kuleta mapinduzi makubwa na mafanikio lukuki katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja ambapo amewataka wadau wote kuishi katika falsasa zake ili kuenzi kwa ufasaha maono na nia njema ya Mhe. Rais. Kauli hiyo ameitoa leo Machi 29,2022 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya mafanikio ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kipindi cha mwaka moja tangu aingie madarakani Machi 19 mwaka jana. Amekemea vitendo vya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakitumia nafasi walizonazo vibaya kwa kujinufaisha wenyewe au kuhujumu maendeleo ya michezo wanayoisimamia. “Viongozi wenzangu niwaombe na kuwasihi sana tusimuangushe Mhe. Rais, bali Tuunge Mkono Juhudi zake, Nia njema na Uthubutu mkubwa aliounyesha katika kuleta mapinduzi kwenye sekta yetu na tuuenzi kwa vitendo.” Amefafanua, Mhe. Mchengerwa. Amesema kama Waziri mwenye dhamana y...

Wadau wa michezo wammwagia sifa Rais Samia katika mwaka moja

Image
  Na. John Mapepele Watoa mada mbalimbali kwenye kongamano la kuelezea mafanikio ya michezo wametoa shuhuda na kupongeza mageuzi na mapinduzi makubwa huku wakisema  mama Samia ameupiga mwingi na kuondoka nao. Aliyeanza ni Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi ambaye amesema Mhe. Rais amekuwa na utashi wa kisiasa kwenye michezo, amefanya uwekezaji mkubwa na kuboresha na kujenga  miundombinu za michezo. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi amefafanua kuwa kutokana na maono makubwa ya Mhe. Rais timu yao imefuzu kwenda kombe la dunia. Aidha, ameongeza kuwa kutokana na utashi huo Mhe. Rais amefungua ajira kubwa za kitaifa na kimataifa kwa wachezaji walemavu. Amesema hadi sasa wachezaji wanne (4) wameshapata timu katika mataifa mbalimbali duniani. Kaimu Katibu Mkuu  wa Shirikisho la Riadha  Jackson  Ndaweka amesema mashindano ya taifa ya riadha  yameweza kufanyika kwa mafanikio makubwa. "Tunashukuru sana mama sasa tumean...

WIZARA NA WADAU WA MICHEZO WAMPA TANO RAIS SAMIA

Image
  Na. John Mapepele Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini leo Machi 29, 2022, wanaadhimisha kilele cha wiki ya Rais Samia ikiwa ni kampeni maalum ya kuelimisha umma, kujadili na kutafakari mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mwaka mmoja wa utendaji wake  tangu aingie  madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 19, mwaka jana. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ndiye Mgeni Rasmi atakayeongoza kongamano hilo la michezo katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Michezo. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa nane mchana na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo. Yusuph Singo Omary, wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sa...

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO

Image
 

Program ya SAMIA CUP- Mtaa kwa mtaa yaiva – Mhe Mchengerwa

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema mwongozo wa program ya michezo na sanaa ya mtaa kwa mtaa imekamilika na utawasilishwa kwenye kikao kazi cha maafisa utamaduni na michezo kinakachofanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili 2022 jijini Dodoma.  Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Machi 26,2022 mara baada ya  ziara yake ya kikazi aliyoambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi kukagua miundombinu mbalimbali ya uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa chumba maalum cha mazoezi ya viongo (Gym) baada ya kupata wasilisho kuhusu program mtaa kwa mtaa  kutoka Idara ya Maendeleo ya Michezo na Baraza la Michezo (BMT) nchini. Mhe. Mchengerwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeamua kuratibu na kuendesha mashindano ya michezo ya kitaifa  yatakayojumuisha  michezo mbalimbali ambayo yataanzia  katika ngazi ya mtaa na kujulikana  kwa jina la SAMIA CUP -Mtaa kwa Mtaa...
Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema mwongozo wa program ya michezo na sanaa ya mtaa kwa mtaa imekamilika na utawasilishwa kwenye kikao kazi cha maafisa utamaduni na michezo kinakachofanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili 2022 jijini Dodoma.  Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Machi 26,2022 mara baada ya  ziara yake ya kikazi aliyoambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi kukagua miundombinu mbalimbali ya uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa chumba maalum cha mazoezi ya viongo (Gym) baada ya kupata wasilisho kuhusu program mtaa kwa mtaa  kutoka Idara ya Maendeleo ya Michezo na Baraza la Michezo (BMT) nchini. Mhe. Mchengerwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeamua kuratibu na kuendesha mashindano ya michezo ya kitaifa  yatakayojumuisha  michezo mbalimbali ambayo yataanzia  katika ngazi ya mtaa na kujulikana  kwa jina la SAMIA CUP -Mtaa kwa Mtaa...

Diamond apongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuwasaidia wasanii, kurejesha tuzo

Image
  Na. John Mapepele Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi na  Msanii maarufu ndani na nje ya Bara la Afrika, Diamond Platinum amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe,  Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwaunganisha  wasanii ili sekta ya Sanaa iweze kuwanufaisha. Diamond amesema haya leo Machi 25, 2022 mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa alipotembelea  Kampuni ya Wasafi inayomiliki rebo ya Wasafi, Wasafi TV na Wasafi FM redio kwa lengo la kukagua  kazi za Sanaa. Amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni imefanya mapinduzi makubwa  katika sanaa kwa  kubuni mikakati mbalimbali ya kuwaunganisha na kuwanufaisha wasanii. Miongoni mwa mikakati ameitaja mizuri ya Serikali kuwa ni pamoja na  kurejesha tuzo za muziki. Kwa  upande wake Mhe. Mchengerwa amesema Serikali imeshatenga  fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye Sanaa ili wasanii waweze kunufa...

SEKTA ZA BURUDANI ZINA MCHANGO MKUBWA- MHE. MCHENGERWA

Image
  Na.  John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotoa mchango mkubwa wa fedha katika taifa kutokana na sekta za burudani. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Machi 24, 2022 wakati alipokuwa akiwasilisha  maelezo ya rasimu  ya mpango wa bajeti ya Wizara  kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa  Kamati ya  Kudumu ya Bunge  ya  Huduma  na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.   Amesema  tafiti zilizofanywa na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC) katika nchi za Afrika, sekta za burudani na vyombo vya mawasiliano (Entertainment and Media (E&M), An African perspective) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2022 zinaonyesha kuwa sekta hizo  zinatoa mchango mkubwa wa kifedha katika nchi hizo.  “Katika kipindi cha mwaka 2017 mapato ya ujumla kutokana na sekta za burudani na vyombo vya mawasiliano (Entertainment...

Maafisa Utamaduni na Michezo nchi nzima kupewa mafunzo ya kusaka vipaji mtaa kwa mtaa- Mhe. Mchengerwa

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara imeandaa kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo  wote nchi nzima ili kuwapa mafunzo maalum ya kusimamia na kutekeleza  mpango wa kitaifa wa kuibua vipaji utakaoanzisha  ligi kuanzia  kwenye  ngazi ya Kijiji na mtaa  hadi taifa  ili kupata timu bora za taifa  katika michezo mbalimbali. Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Machi 22, 2022 alipokuwa akifungua semina kwa Kamati ya  Kudumu ya Bunge  ya  Huduma  na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma  na amesema kikao hicho kitafanyika Aprili 5-6, 2022 mjini Dodoma na kinatarajiwa  kufunguliwa na Waziri Mkuu Mhe, Kassim Majaliwa. Amefafanua kuwa ligi hii ni mpango maalum wa Serikali wa kuendeleza michezo ambao unatekeleza dhana ya kuibua wachezaji kuanzia chini ya mtaa kwa mtaa.  Mbali na kuanzisha ligi hizo Mhe. Mchengerwa ametaja mambo mengine ma...

BASATA, COSOTA TOKENI WASAIDIENI WASANII, HAKUNA MSANII MKUBWA KULIKO NCHI -MHE. MCHENGERWA

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amezielekeza Taasisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA) kukamilisha zoezi la kuwasajili wasanii  wote    hususan  wale wa kubwa ambao  bado hawajasajiliwa  huku akisisitiza kuwa hakuna msanii  mkubwa  kuliko nchi. “Leo  nataka  niwaelekeze BASATA na COSOTA na sitaki  kurudia rudia jambo  hili.Hatutegemei  kusikia  eti wamesajiliwa wasanii wachache, au kusikia msanii  mkubwa  hajasajiliwa tutaanza kuhoji uwezo wa wewe tuliokupa  dhamana”. Amefafanua Mhe Mchengerwa  Mhe. Mchengerwa ametumia muda wa takribani masaa matatu kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali hususan ya wasanii na kutoa maelekezo ya kusaidia wasanii wote nchini na kuwaunganisha ili waweze kufaidika na kazi zao k alipokuwa mgeni rasmi kwenye kikao cha Baraza la wafanya kazi  la Wizara yake Machi 21, jijin...

Mhe. Mchengerwa amtaka Mkandarasi kuongeza kasi, kufanya kazi usiku na mchana

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  amemtaka Mkandarasi wa Jengo la Wizara la Mtumba jijini Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi na  kufanya kazi mchana  na usiku ili kwenda na ratiba hatimaye kukamilisha ujenzi wa Jengo hilo kwa wakati uliopangwa kwa kuwa Serikali omeshatoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo. Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo Machi 21, 2022 wakati alipotembelea kukagua  eneo la ujenzi wa Ofisi  hizo ambapo hakuridhishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea kwa kuwa upo nyuma ya muda. Ujenzi huo wa ghorofa 6  unatekelezwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) chini ya Mkandarasi Mshauri Wakala wa Majengo nchini (TBA). "Naomba sana Mkandarasi uchape kazi, hakuna sababu ya wewe kutokwenda na ratiba ya kazi zako kwa kuwa Serikali imeshatoa fedha zote za kazi hiyo" Amehoji Mhe. Mchengerwa. Kwa upande mwingine, amesema amesikitishwa kuona taasisi za Serikali zimeaminiwa  na  kupew...

Tuyatekeleze maelekezo ya Mhe. Rais kwa kasi na weledi- Mhe. Mchengerwa

Image
  Na Eleuteri Mangi-WUSM, Dodoma Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake imejipanga  kutekeleza maelekezo 16 ya kisekta kwa kasi na weledi katika mwaka wa fedha 2022/2023  ili kuwahudumia wananchi. Waziri Mchengerwa ametoa kauli hiyo Machi 21 Jijini Dodoma wakati akiwa mgeni rasmi kwenye kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa  mwaka 2022 ambapo wizara imedhamiria kuyatekeleza kwa ufanisi kwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanaitegemea wizara hii kwa namna moja au nyingine. Mhe. Mchengerwa amesema maelekezo hayo yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa ambayo lengo lake ni kuwahudumia Watanzania. “Kila mmoja awajibike kwenye eneo lake, tukijifungia  ofisini hatutafikia malengo na matarajio ya Serikali, twende kuwahudumia wananchi, tuwafikie na kuwapa faida ya Serikali yao”. amesisi...

Mhe. Mchengerwa aipongeza Serengeti Girls kwa kuibamiza Botswana 4-0, kufuzu kombe la dunia

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza Timu ya Taifa U-17 Serengeti Girls kwa  kuishinda timu ya Taifa ya Botswana mabao 4-0 katika  mchezo wa kufuzu kucheza kombe la Dunia 2022 nchini India.  Mhe. Mchengerwa amesema  timu ya Serengeti Girls inasitahili pongezi kwa kuwa imeendelea kuiheshimisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa. "Nilipoitembelea kambini wiki iliyopita  huko Zanzibar nilifanya vitu viwili; niliwapa jina rasmi la Serengeti Girls na niliwapa mikakati, ninafurahi kuona wamelitendea haki jina hilo na mikakati tuliyowapa wameitekeleza". Ameeleza Mhe. Mchengerwa. Timu ya Taifa ya Wanawake U17 ya Serengeti Girls imeweza kufuzu mzunguko unaofuata baada ya kuwatoa Botswana kwa jumla ya magoli 11 kwa 0 baada mechi ya awali iliyopigwa Zanzibar kushinda 7-0 na  jana marudiano kushinda magoli 4-0 yaliyofungwa na Neema Paul 1 na Clara Luvanga 3. Baada ya mchezo huu mchezo unaofuata Serenge...