YAKUBU- VYUO VIKUU ENDELEENI KUANDAA MATAMASHA
Na. John Mapepele Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ametoa wito kwa vyuo vikuu nchini vinavyofundisha sanaa kuandaa matamashaa ya utamaduni ili kuibua vipaji vitakavyoleta ajira kwa vijana. Yakubu ameyasema haya leo Januari 29, 2022 alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa wakati wa kilele cha tamasha la sanaa la kuadhimisha miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam toka kuanzishwa kwake. Amefafanua kwamba matamasha haya yanasaidia kuibua vipaji na kuendeleza utamaduni wa taifa letu. Aidha, amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa nafasi ya washindi watatu katika tamasha hili kushiriki kwenye tamasha kubwa la kitaifa la Serengeti litakalofanyika Dodoma mapema mwezi Machi 2022. Amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais katika kuendeleza Utamaduni na dira yake ya 2061 na mikakati yake ya kuimaris...